Bao la Iheanacho lailaza Tanzania
Nyota ya Kelechi
Iheanacho inaendelea kung'aa ,kwani wiki moja tu baada ya kutia saini
kandarasi ya malipo ya pauni 85,000 kwa wiki na kuwa mchezaji anayelipwa
juu zaidi nchini Nigeria ameonyesha umahiri wake.
Bao la mda wa
ziada la mshambuliaji huyo wa Manchester City ndilo lililoweza kubaini
mbivu na mbichi dhidi ya Tanzania katika mchuano wa kufuzu kwa kombe la
bara Afrika 2017.Kutoka kwa kona fupi,mshambuliaji huyo alijitafutia mwanya akiwa karibu na lango la Tanzania star na kuwachilia mkwaju uliopiga mwamba wa goli na kumwacha kipa wa Tanzania bila jibu.
No comments