Video Of Day

Breaking News

Trump atishia kumualika mpenzi wa zamani wa Clinton,,,,,,,,,,,,

WILLYD193.BLOGSPOT.COM

Trump atishia kumualika aliyekuwa mpenzi wa Clinton
Image captionTrump atishia kumualika aliyekuwa mpenzi wa Clinton
Donald Trump ametishia kumualika mwanamke ambaye alikuwa mpenzi wa Bill Clinton akiwa kwenye ndoa na Hillary Clinton.
Trump amesema atamualika Gennifer Flowers akae mbele kabisa, kwenye mjadala baina yake Trump na mpinzani wake wa kugombea urais, Hillary Clinton, hapo kesho.
Bwana Trump alisema hayo, kujibu matamshi ya bilioneya anayeshindana naye, Mark Cuban ambaye alisema, kampeni ya Clinton imempa kiti cha mbele katika mjadala huo.
Gennifer Flowers anadai alikuwa mpenzi wa Bill Clinton akiwa kwenye ndoa na HillaryImage copyrightAP
Image captionGennifer Flowers anadai alikuwa mpenzi wa Bill Clinton akiwa kwenye ndoa na Hillary
Gennifer Flowers, mrembo wa zamani, amejibu kwenye Twitter, kwamba amepokea mualiko wa Bwana Trump.
Haijulikani kama Trump atafuata tishio lake hilo au la

No comments