Video Of Day

Breaking News

Rais Magufuli apokea taarifa ya mradi mkubwa wa gesi

Rais Dk John Magufuli amepokea taarifa ya maendeleo ya mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika gesi asili (LNG Plant) kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la Likong’o, Mchinga mkoani Lindi.


 1 (1)


  Rais Magufuli akisalimia na muakilishi wa Statoil ya nchini Norway kabla ya kupokea taarifa ya ujenzi mkubwa

Ameupokea ujumbe huo Jumatatu hii ikulu jijini Dar es Salaam

.2

Mwakilishi mkazi wa kampuni ya Statoil ya nchini Norway, ambayo ni moja ya kampuni zitakazowekeza katika mradi huo, Oystein Michelsen alimueleza Rais Magufuli kuwa ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 30 sawa na zaidi ya shilingi trilioni 65 za Tanzania na kwamba uzalishaji unatarajiwa kuchukua muda wa zaidi ya miaka 40 baada ya kuanza.
“Serikali ya Norway ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa manufaa ya pande zote na nimeomba serikali ya Tanzania iendelee kutoa ushirikiano ili kufanikisha ujenzi wa kiwanda hicho”,alisema Michelsen.
Rais Magufuli, kwa upande wake alimhakikishia mwakilishi huyo wa kampuni ya Statoil kuwa serikali ya Tanzania ipo tayari kuhakikisha mradi unafanikiwa na kuitaka Wizara ya Nishati na Madini kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kushirikiana na wadau kutoka wizara nyingine kuharakisha mchakato wa kuanza kwa ujenzi wa kiwanda hicho.

No comments